Papa Francis ameongoza maombi mjini Vatican kwa ajili ya wahanga wa shambulio katika shule moja nchini Uganda.
Takriban watu 40 - wengi wao wakiwa wanafunzi - walikatwakatwa, kupigwa risasi na kuchomwa moto hadi kufa katika mji wa Mpondwe, magharibi mwa nchi hiyo siku ya Ijumaa usiku.
Jeshi la Uganda limesema kuwa linawasaka wanamgambo hao kutoka kundi linalojulikana kwa jina la ADF.
Waliwateka nyara wanafunzi sita kabla ya kutoroka kuvuka mpaka na kuingia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Shambulio hilo pia limelaaniwa na rais wa Uganda, Yoweri Museveni ambaye alilitaja kuwa l uhalifu na lisilo na maana.
Familia za baadhi ya waathiriwa zimeanza kuwazika wapendwa wao.