Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pande hasimu Sudan zalaumiana kwa kuharibu bwawa la Khartoum

Bwawa La Sudan Lawama Pande hasimu Sudan zalaumiana kwa kuharibu bwawa la Khartoum

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majenerali wa kijeshi wanaoongoza pande mbili hasimu yaani Jeshi wa Sudan (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kila mmoja anamtupia lawama mwenzake kuhusu kuharibiwa daraja kwenye bwawa la Jabal Awliya la kusini mwa mji mkuu, Khartoum.

Katika sehemu moja ya lawama zake kwa RSF, jeshi la Sudan limesema: "Ikiwa ni muendelezo wa uharibifu wake dhidi ya miundombinu ya Sudan, mizinga ya wanamgambo waasi na magaidi imesababisha uharibifu mkubwa kwenye daraja la bwawa la Jabal Awliya alfajiri ya Jumamosi."

Kwa upande wake, RSF wamejibu tuhuma hizo za jeshi la Sudan kwa kusema kuwa ni jeshi hilo ndilo lilifanya uharibifu huo.

Sehemu moja ya taarifa ya RSF imesema: "Uharibifu wa daraja la Jabal Awliya ni uhalifu kamili wa kivita uliofanywa na jeshi wa kuangamiza miundombinu muhimu yenye manufaa kwa watu wa kawaida na vifaa vya kibinadamu." Uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi unazidi kuiangamiza Sudan

Mapigano yamekuwa yakiendelea kati ya majenerali wa kijeshi wanaoongoza vikosi vya SAF na RSF kwa ajili ya kulidhibiti eneo la Jabal Awliya la kusini mwa Khartoum kwa wiki ya pili sasa.

Eneo hilo linajumuisha kituo cha Jeshi la Anga cha Al-Nujoumi ambacho ni moja ya vituo vinne muhimu vya anga nchini Sudan. Ni katika eneo hilo pia ndipo lilipo bwawa kubwa la Jabal Awliya. Kuharibiwa daraja la bwawa hilo kumeongeza hatari ya kuzuka mafuriko makubwa ya Mto Nile.

Wiki iliyopita, vikosi vya RSF vilidai kulidhibiti bwawa la Jabal Awliya na kituo cha anga cha Al-Nujoumi, lakini vikosi vya SAF vilikanusha madai hayo na kusema kuwa eneo hilo lote lilikuwa chini ya udhibiti wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live