Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Panda shuka za Rais Museveni nchini Uganda

Shambulio La Al Shabab Liliwatia Hofu Wanajeshi Wa Uganda Rais Museveni Panda shuka za Rais Museveni nchini Uganda

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Septemba 15, 1944, Magharibi mwa nchi ya Uganda, nyota ya Yoweri Kaguta Mseveni ilichomoza na takribani miaka 40 baadae Mseveni alichukua nchi baada ya kile kilichoitwa vita ya msituni akiwa na kundi lililojulikana kama National resistance Army

Museveni aliongoza vita ya msituni dhidi ya serikali ya Milton Obote ambaye alikuwa madarakani kwa wakati huo akiongoza Uganda toka mwaka 1980-1985 pamoja na mtangulizi wake Idd Amin ambaye aliongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 1971-1979.

Tangu hapo Mseveni amekuwa akishinda uchaguzi mkuu kwa kugombea nafasi ya urais tangu mwaka 1996-2021 na kushika nafasi hiyo hadi sasa akiwa madarakani kama rais wa Uganda.

Katika uongozi wake yapo mambo mazuri na yale ambayo yaliweka Dosari katika uongozi wake.

MAMBO MAZURI YA MSEVENI

Mara tu baada ya kuingia madarakani kwa mara ya kwanza alifanya mambo mazuri ambayo yalimtofautisha sana na watangulizi wake waliopita.

Alifanikisha mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UKIMWI ambao kwa wakati huo ilikuwa moja ya tatizo kubwa zaidi nchini humo kwa kufuata sera za wakati huo za benki ya dunia na shirika la Fedha Duniani (IMF),jambo ambalo hata viongozi wa mataifa ya Magharibi walimpongeza

Pia Alikuta nchi ikiwa katika hali mbaya kiuchumi na hususani uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini mpaka sasa uchumi wan chi hiyo umeonekana kuimarika na kipato cha mtu mmoja mmoja kimeongezeka .

Kingine alichofanikiwa ni kuimarisha ulinzi na usalama dhidi ya waganda na kuwaongoa katika migogoro ya wenyewe kwa wenyewe na hata matishio ya kigaidi ambayo yalikuwapo wakati tu anaingia madarakani hususani kundi la Lord resistance Army (LRA)ambalo lilikuwa tishio kwa wakati huo na alifanikiwa kupambana nalo.

Na hivi karibuni ni mapambano yake dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19 ambao alifanikiwa kupambana nao lakwini kwa sasa yeye pia anasumbuliwa na ugonjwa huo.

Lakini licha mambo mazuri mengi ambayo ameweza kuyafanya kwa taifa lake kumekuwepo na changamoto ambazo zilitajwa kama dosari ambazo zinatia Doa uongozi wake.

CHANGAMOTO KATIKA UONGOZI WA RAIS MSEVENI MADARAKANI

Miongoni mwa changamoto kubwa ambayo imekuwa ikielezwa hasa na wapinzani wake nchini humo ni matumizi ya nguvu na ubabe hasa wakati wa uchaguzi na wamekuwa wakilalamika kupigwa kuteswa na kutishwa vikali na miongoni mwa viongozi ambao wamekuwa wakilalamika sana ni pamoja na BOBI WINE (Robert Chagulanyi ) na KIZA BESIGYE ambaye huyu, nikikurudisha nyuma kidogo alitaka kujiapisha mwenyewe kuwa rais wa Uganda kwa kuamini kuwa alishinda uchaguzi ikiwa ni siku moja kabla ya Rais Mseveni Kuapishwa rasmi mwaka 2016.

Jingine ni kukaa kwenye nafasi hiyo ya Urais kwa muda Mrefu jambo ambalo limekuwa litafsiriwa na jamii za kimataifa kama mtu anaeminya Demokrasia kwa kutoruhusu wengine kushika nafasi hiyo na kushindwa kuachia madaraka ,na mpaka sasa Mseveni ndie Rais ambae amekaa muda mrefu zaidi madarakani akihudumu kwama rais wan chi hiyo.

HALI ILIVYO SASA

Kwa sasa Mseveni anakabiliwa na changamoto ya kupata shinikizo kubwa toka mataifa ya magharibi baada ya kupitisha muswada unaohusu adhabu kwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na hta kukabiliwa na tishio la kusitishwa kwa misaada nchini humo kutokana na hilo.

Pia Changamoto ya afya yake mara tu baada ya kutangaza kuwa amepeata maambukizi ya ugonjwa wa Uviko 19 na kuwepo kwa taarifa nyingi kuhusu afya yale licha ya kwamba kwa mujibu taarifa rasmi kutoka ikulu ya Uganda zikionesha anaendelea vizuri .

Mseveni anatajwa miongoni mwa viongozi wa Afrika ambao wamekuwa wakisimamia misimamo yao nan i ngumu kutumbishwa na yeyote Yule.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live