Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Palestina yaitaka AU kuindolea Israel hadhi ya ungalizi

Palestina Afrika Waziri Mkuu wa Palestina Mohammed Shtayyeh

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Palestina Mohammed Shtayyeh ameuhimiza Umoja wa Afrika kuifuta idhini ya kuikaribisha Israel kama mjumbe mwenye hadhi ya uangalizi kwenye umoja huo akisema taifa hilo halipaswi kupatiwa heshima hiyo.

Wito wa kiongozi huyo wa Palestina umetolewa wakati viongozi wa mataifa ya Afrika wanakutana mjini Addis Abbaba kwa mkutano wa kilele wa siku mbili utakaogubikwa kwa sehemu kubwa na wimbi jipya la mapinduzi ya kijeshi barani humo na janga la virusi vya corona.

Shtayyeh amesema uamuzi wa kuipa Israel hadhi maalum ya uangalizi kwenye Umoja huo ambao ulipitishwa mwaka jana na mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat haukubaliki kutokana rikodi ya Israel ya kuwakandamiza watu wa Palestina.

Mkutano huo wa kilele huenda ukashuhudia kupigwa kura ya kuamua iwapo unaunga mkono au kupinga uamuzi kuhusu Israel

Chanzo: www.tanzaniaweb.live