Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Oscar Pistorius kukutana na wazazi wa mwathiriwa Reeva Steenkamp

Pp Pistorius 2 Getty Oscar Pistorius kukutana na wazazi wa mwathiriwa Reeva Steenkamp

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: BBC

Oscar Pistorius amehamishiwa gereza tofauti kukutana na familia ya Reeva Steenkamp, mwanamke aliyemuua mwaka 2013. Idara ya magereza ya Afrika Kusini imethibitisha taarifa hiyp, ikisema ni sehemu ya mchakato wa ukarabati unaofanyika kabla ya mwanariadha huyo wa zamani wa Olimpiki ya walemavu kuzingatiwa kwa msamaha.

Idara hiyo pia imethibitisha kwamba alihamishwa hadi katika gereza katika mji wa bandari wa Gqeberha, uliyopo Cape ya Mashariki, ili kukutana na wazazi wa Reeva Steenkamp, ​​wanaoishi karibu.

Mapema mwaka jamaa ya Steenkamps walikiri kupokea barua kutoka kwa mwanamume aliyemuua binti yao. Lakini walidokeza kwamba majuto yake yalikuwa ya kujitakia'

Maafisa wa Afrika Kusini hawajaonyesha dalili ya muda gani mchakato huo - unaojulikana hapa kama mazungumzo ya mwathirika-mkosaji - utaendelea. Lakini itazingatiwa wakati bodi ya msamaha itakapokutana ili kuamua ikiwa Pistorius aachiliwe kutoka gerezani.

Reeva Steenkamp alipigwa risasi nne akiwa amejificha nyuma ya mlango wa bafuni mnamo Februari 2013.

Awali Jaji alimpata Pistorius na hatia ya kuua bila kukusudia, ambayo ilibadilishwa na kuwa mauaji, baada ya kukata rufaa.

Mwanariadha huyo ambaye miguu yake yote miwili ilikatwa akiwa mtoto mchanga, alisema aliamini alikuwa akimpiga risasi mvamizi.

Chanzo: BBC