Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onyo la Umoja wa Mataifa kuhusu kuongezeka vifo katika nchi ya Somalia

Somalia: Mapigano Makali Yaibuka Baina Ya Polisi Na Kundi La Wanamgambo Onyo la Umoja wa Mataifa kuhusu kuongezeka vifo katika nchi ya Somalia

Sat, 21 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Somalia ameonya kuhusu kuongezeka kwa idadi ya vifo vya raia vilivyotokea mwaka jana katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika iliyokumbwa na ghasia za makundi ya siasa kali.

Catriona Laing, mwanadiplomasia wa Uingereza aliyechukua wadhifa huo mapema mwaka huu, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa hali hiyo imesababishwa na uasi wa wanamgambo wa kundi la al-Shabaab na mapigano katika eneo lililojitenga la Somaliland.

Laing alisema tangu kuanza kwa mwaka huu, raia wapatao 1,289 wameuawa.

Operesheni dhidi ya al-Shabaab zimeshtadi wakati huu ambapo Umoja wa Afrika unaendelea na awamu ya pili ya kuondoa wanajeshi wa umoja huo (ATMIS) kutoka nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Al-Shabaab ni kundi lenye mafungamano na mtandao wa al-Qaeda na limefanya operesheni nyingi za kigaidi ambazo zimeua mamia ya watu barani Afrika.

Wanamgambo wa al-Shabab wa Somalia

Magaidi wa al-Shabaab wamekuwa wakishambulia mara kwa mara wanajeshi wa serikali na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika, pamoja na watu wa kawaida huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, na kufanya operesheni kadhaa za umwagaji damu katika maeneo mengine barani humo.

Hayo yanajiri huku mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika wiki ya pilii ya mwezi huu yamesababisha mamia ya kuyahama makazi yao katika wilaya ya Baidoa ya kusini magharibi mwa Somalia.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mvua hizo kubwa na mafuriko yamekuja kufuatia misimu mitano ya ukame ambayo imesababisha vifo vya zaidi ya Wasomali milioni 1.4 na mifugo milioni 3.8 tangu katikati ya mwaka 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live