Rais wa Nigeria, Bola Tinubu ametangaza nyongeza ya mshahara kwa miezi sita hadi kima cha chini cha mshahara, huku wafanyakazi wakitarajiwa kuanza mgomo kwa muda usiojulikana.
Ongezeko hilo la $32 ambayo ni sawa na Tsh 80,320 la mshahara wa chini wa kila mwezi wa hadi $70 sawa Tsh. 175,700 lilitangazwa na Tinubu huku akiahidi kuharakisha uanzishaji wa mabasi ya bei nafuu yanayotumia gesi, ili kusaidia unafuu wa usafiri kutokana na gharama za mafuta zilizopanda.
Vyama vya Wafanyakazi vikitaka mshahara uongezwe hadi Tsh. 640,050 ili kusaidia kukabiliana na ongezeko kubwa la gharama za maisha tangu Rais Tinubu aondoe ruzuku ya Mafuta.
Hata hivyo, Vyama Vikuu vya Wafanyakazi Nchini humo vya NLC na (TUC, vimesema wataendelea na mgomo usio na kikomo kuanzia Jumanne, Oktoba 3, 2023 huku Viongozi wake wakisisitiza kuwa Serikali imeshindwa kushughulikia masaibu yaliyosababishwa na kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta
Juni 2023, nchi hiyo pia iliachana na mpango wake wa fedha wa kuruhusu biashara ya uhuru hali liyosababisha anguko kubwa zaidi katika historia ya naira na kufanya maisha kuwa magumu kwa Wanigeria kutokana na mfumuko wa bei uliopanda kutokana na kuongezeka kwa gharama ya uagizaji bidhaa kutoka nje.