Ongezeka la Bei ya Kopa kwa nchi ya Zambia, umekadiriwa kuongeza Uchumi wa nchi hiyo kwa asilimia 1.5%. Ongezeko hilo limesaidia kuimarisha uwezo wa kuzalisha umeme.
Nchi ya Zambia yenye utajiri wa Madini katika Jimbo la Kusini, Mkoa wa Magharibi na Mkoa wa Kaskazini-Magharibi imepiga kura huku mategemeo mengi ya vijana yakiwa kudumisha hali ya uchumi kwa Viongozi wanaowachagua.
Wakazi katika maeneo hayo wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kwamba hakuma maendeleo ya kiuchumi licha ya kuwa na migodi mikubwa ya madini.
Mdororo wa Uchumi umeikumba nchi hiyo Tangu mwaka 2011 Rais Edgar Lungu alipoingia madarakani na hii inaleta taswira kwamba Mgombea Hakainde Hichilema wa Chama cha Upinzani wa chama cha United Party for National Development (UPND).
Nchi hiyo pia inadaiwa na wakopeshaji wa kigeni deni linalokadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni 12 sawa na (£8.6bn).
Hii inamaanisha kuwa serikali inatumia hadi asilimia 30 ya mapato yake kulipa riba kulingana na shirika la kimataifa la S&P linalokadiria viwango vya madeni.
Mwaka jana Zambia ilikosa kulipa deni, na kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kushindwa kulipa deni lake wakati wa janga la corona. Pia inakabiliwa na changamoto ya kulipa mikopo mingine.