Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ondinga aungana na waandamanaji asema wataacha gharama zikishuka

ODINGA MOJA Ondinga aungana na waandamanaji asema wataacha gharama zikishuka

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amejiunga na waandamanaji mjini Nairobi wanaopinga kupanda kwa garama ya maisha.

Akishangiliwa na umati wa wandamanaji waliokuwa wakipaza sauti, 'Unga!, Unga!, Unga!...'' Bw Odinga amesema maandamano yataendelea hadi garama ya maisha itakaposhuka.

Polisi wamerusha vitoa machozi msafara wa magari yaliyokuwa yamembeba Raila Odinga na wanasiasa wengine, vyombo vya habari vya nchini vimeripoti.

Tangu majira ya asubuhi polisi wamekuwa wakikabiliana na waandamanaji kwa kuwarushia mambomu ya kutoa machozi, na kuwapiga kwa maji, huku waandamanaji wakiwarushia mawe na kufunga barabara.

Hizi ni baadhi ya picha za matukio yaliyojiri katika Jumatatu ya maamdamano ya upinzani kutoka kwa waandishi wetu:



Chanzo: Bbc