Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ondinga atangaza maandamano ya kitaifa Kenya

Ondinga Atangaza Maandamano Ya Kitaifa Kenya Ondinga atangaza maandamano ya kitaifa Kenya

Thu, 9 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Kinara wa muda mrefu wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kuanzishwa kwa shughuli nyingi za migomo na maandamano ya kitaifa.

Bw Odinga anasemavuguvugu la ‘Movement for Defense of Democracy’ litaweka shinikizo kwa utawala wa Rais William Ruto alioutaja kuwa ‘’usio halali’’.

Bw. Odinga aamewataka wafuasi wake kutii wito wa kukaidi kwa kufanya migomo, maandamano ya amani na maombi.

"Kuanzia siku ya leo tunaanza sasa kipindi kipya cha ukombozi…tunaanza chama chetu cha ukombozi wa taifa let chama cha kutetea ukombozi wa taifa leo na tumesema tutatumia njia za kisheria na kikatiba," amesema Bw Raila.

Akiorodhesha malalamiko ambayo serikali ilikosa kushughulikia katika makataa yake ya siku 14 yaliyotimia hii leo, Odinga alimshutumu Rais Ruto kwa kuiteka idara ya mahakama, ukabila, ufisadi na uongozi mbaya.

Vuguvugu hilo jipya linapanga kufanya mikutano ya kupinga serikali kote nchini itakayofikia kilele kwa maandamano makubwa katika mji mkuu tarehe 20 Machi.

Odinga ambaye alishindwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka uliyopita na William Ruto alimshutumu Ruto kwa kushindwa kudhibiti gharama ya maisha na mageuzi ya uchaguzi.

Chanzo: Bbc