Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#OmicronVirus: Ramaphosa arejea kazini baada ya kupona Corona

Cyril Ramaphosa?fit=754%2C409&ssl=1 Rais Ramaphosa arejea kazini baada ya kuugua Corona

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amerejea kazini baada ya kumaliza wiki moja ya kujitenga baada ya kukutwa na virusi vya Corona, ofisi yake imethibitisha hilo.

Ramaphosa, ambaye alipewa chanjo ya Johnson & Johnson mnamo Februari, alipimwa na na kukutwa na maambukizi ya COVID-19 mnamo Desemba 12 na akapokea matibabu ya dalili zisizo kali.

“Rais amerejea kazini na ataongoza kikao cha mwisho cha baraza la mawaziri kwa 2021 siku ya Jumatano,” ilisema taarifa ya ofisi ya Rais.

Katika siku chache zilizopita, milipuko ya kitaifa inayoaminika kuhusishwa na aina mpya ya kirusi cha Omicron imekuwa ikiambukiza zaidi ya watu 20,000 kwa siku, ingawa idadi ya maambukizo mapya yaliyorekodiwa ilipungua wikendi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live