Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa wa UN atimuliwa Burkina Faso

Afisa UN Burknadeee.jpeg Ofisa wa UN atimuliwa Burkina Faso

Mon, 26 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso imemuamuru mratibu wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa, Barbara Manzi kuondoka nchini humo mara moja.

Taarifa ya wizara ya mambo ya kigeni imemtangaza Manzi, mkazi wa Umoja wa Mataifa na msaidizi wa masuala ya kibinadamu katika Taifa hilo la Afrika Magharibi kuwa mtu asiyefaa.

Ingawa hakuna sababu iliyotolewa katika taarifa ya kufukuzwa kwake, Waziri wa Mambo ya nje, Olivia Rouamba akizungumza kwenye televisheni ya Taifa ya nchi hiyo siku ya Ijumaa alisema Manzi alikuwa ametoa tahadhari kuhusu ukosefu wa usalama katika mji mkuu, Ouagadougou, bila kutoa ushahidi.

Takriban watu milioni mbili wameyakimbia makazi yao na kuishi katika kambi za muda, nyingi zinazosimamiwa na Umoja wa Mataifa, ambazo ziko katika maeneo kame ya mashambani.

Vurugu hizo zimeendelea kwa takribani miaka saba, zimeelekezwa kaskazini na mashariki na kuzorotesha uchumi wa ndani na kusababisha njaa na kuzuia ufikiaji wa mashirika ya misaada.

Umoja wa Mataifa hutoa huduma muhimu, ikiwa ni pamoja na kusambaza chakula kwa maelfu ya watoto wenye utapiamlo.

Manzi, ambaye ana uzoefu wa muda mrefu katika shughuli za kibinadamu katika nchi zinazoendelea, aliteuliwa kushika wadhifa huo nchini Burkina Faso mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live