Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Odinga amtuhumu Ruto mauaji ya waandamanaji wa Gen Z

Gen Z Rutoo Odinga amtuhumu Ruto mauaji ya waandamanaji wa Gen Z

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu mstaafu na aliyekuwa mgombea Urais wa Kenya katika Uchaguzi Mkuu 2022, Raila Odinga amemtuhumu Rais William Ruto kuhusika na mauaji ya waandamanaji wa Gen Z yaliyotokea jana Juni 25, 2024.

Aidha, Odinga kupitia taarifa yake kwa umma aliyoitoa leo Jumatano Juni 26, 2024 ametaka maandamano hayo yamalizwe kwa njia ya mazungumzo na si nguvu kama inavyofanya Serikali ya Kenya.

“Leo nchi yetu inalipia gharama kubwa kwa ukaidi wa Serikali. Mambo ambayo yalipaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo na unyenyekevu yameharibika na kushuhudiwa vitu ambavyo havijawahi kutokea kwa miaka 61 ya Uhuru.

“Nimesikitishwa sana na ukandamizaji mbaya dhidi ya vijana, waandamanaji wa amani wanaotumia haki yao ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza.

Nimesikitishwa na mauaji, kukamatwa, kuwekwa kizuizini na ufuatiliaji unaofanywa na polisi kwa wavulana na wasichana wanaotafuta tu kusikilizwa kuhusu sera za ushuru zinazoiba maisha yao ya sasa na ya baadaye,” amesema Odinga na kupitia taarifa yake.

Waandamanaji wa Kenya, wanapinga muswada wa sheria ya fedha na hali ngumu ya maisha.

Hata hivyo, Rais Ruto jana alihutubia Taifa hilo, akisema waandamanaji wa Gen Z waliovamia jengo la Bunge walikuwa na viashiria vya kiuhalifu na hayakuwa maandamano ya amani.

“Navishukuru vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi waliyoufanya leo (jana) ya kulinda amani…sio sawa wahalifu kujifanya waandamanaji wa amani, tutalimaliza jambo hilo bila kuleta madhara,” alisema Rais Ruto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live