Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Odinga amkumbuka Mkapa alivyosuluisha vurugu za Uchaguzi 2007-2008

ZyV6L9EBgRRAILA CRYING WITH KALONZO 660x400 Odinga amkumbuka Mkapa alivyosuluisha vurugu za Uchaguzi 2007-2008

Fri, 24 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Kiongozi wa Chama cha Upinzani cha ‘Orange Democratic Movement (ODM)’ cha Kenya, Raila Odinga ameomboleza kifo cha Rais Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya 3, Benjamin Mkapa kilichotokea usiku wa kumkia leo kwa kumkumbuka kwa mengi ikiwepo alivyosuluhisha vurugu baada ya uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo 2007 – 2008.

Odinga  “Kenya tunabakiwa na kumbukumbu kubwa kwa namna alivyohusika pamoja na Dkt. Kofi Annan (Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa) na Graca Machel kusaidia nchi hii kurudi katika amani baada ya vurugu kufuatia Uchaguzi Mkuu wa 2007-2008?.

Ameongeza kuwa licha ya upatanisho huo pia Mkapa anakumbukwa kwa kuwa kiongo cha Pan Africanism na ushirikiano wa kusini mwa afrika.

“Mkapa alikuwa rafiki mkubwa wa watu wa Kenya, muumini mkubwa wa Pan Africanism na muamini mkubwa wa ushirikiano wa Kusini-Kusini” Ondinga kwenye ukurasa wake wa Twitter

KABLA HAJAFARIKI, MANENO YA MWISHO YA MKAPA MBELE YA RAIS MAGUFULI

Chanzo: millardayo.com