Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Odinga: Mitumba ni nguo za watu waliokufa

Mitumba Kenya.png Mitumba ni nguo za watu waliokufa

Wed, 8 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mgombea urais wa Kenya Raila Odinga amepuuzilia mbali madai kwamba anataka kusambaratisha biashara ya mitumba akisema kwamba ameeleweka visivyo.

Bw. Raila alisema sekta hiyo haiwezi kufungwa kwasababu inatoa ajira kwa Wakenya wengi.

Haya yanajiri bada ya wapinzani wake kutumia kauli ya kwamba nguo za mitumba zinazovaliwa sana nchini ni za watu waliokufa.

Aliwaambia wapinzani wake wajiepushe na propaganda na kutoa wito kwa washikadau wa mitumba kuwapuuza uvumi unaoenezwa mitandaoni kuhusu kauli aliyotoa kuhusu nguo za mitimba.

Licha ya ya ufafanuzi huo kwa siku ya pili mfulululizo Wakenya wamekuwa waitumia Hashatag ya Mitumba Challenge kuelezea jinsi wamekuwa wakitegemea nguo hizo.

Huku mjadala huo ukiendela mtandaoni Raila ameahidi kuwa utawala wake utaipa nguvu sekta ya biashara ili kuhakikisha wanaoitegemea hawako nje ya biashara.

"Mitumba sio biashara ya mwisho na imetengeneza ajira kwa watu wetu wengi sana nawatetea na kuna watu

Mwanasiasa Charity ngilu ambaye pia ni Gavana wa jimbo la Kitui mashariki mwa Kenya alisema mjadala unaoendelea sasa mitandaoni kuhusu mitumba uliwahi kuangaziwa na Naibu wa Rais wa Kenya William Ruto lakini haukuangaziwa lakini Raila Odinga alipotoa kauli kuhusu nguo hizo kila mmoja anazungumzia.

Mchambuzi wa siasa za Kenya MUtahi ngunyi alisema Rwanda ilisimamisha Mitumba mwaka wa 2018. Sasa Wakenya wanaagiza mitumba kutoka Rwanda. Nguo zilizovaliwa Rwanda hadi zikachakaa. Kwa hivyo nauliza: Je, Baba alisema nini kuhusu Kicomi JEANS kutoka Kenya na mashati ya Rivatex?

Matamshi ya Raila kuhusu nguo za mitumba yalizua taharuki kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumanne.

Akizindua manifesto yake katika uwanja wa Nyayo Jumatatu usiku, kiongozi huyo wa ODM alisema kuwa nguo za mitumba zinazovaliwa na Wakenya ni za watu ambao waliokufa.

"Watu wetu wamevalia tu nguo zinazotoka nje ya nchi ambazo zilivaliwa na watu waliokufa," Raila alisema.

Raila alisema atalenga kukuza tasnia ya vitambaa nchini kwa kuwapa waagizaji mitumba kipaumbele cha kwanza katika uuzaji wa nguo zinazotengenezwa nchini.

"Mimi nasema hatumuondoi mtu nje ya biashara, tutahakikisha wanaoagiza mitumba wanapata soko la bidhaa zinazoenda kutengenezwa hapa nchini," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live