Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Obasanjo: Demokrasia ya Magharibi imefeli barani Afrika

Biden Anasema 'hana Imani' Na Idadi Ya Waliouawa Gaza Obasanjo: Demokrasia ya Magharibi imefeli barani Afrika

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo amesema, demokrasia ya Magharibi imeshindwa kufanya kazi kama mfumo wa serikali barani Afrika kwa sababu iliwekwa na mamlaka za kikoloni.

Obasanjo amesema hayo katika mkutano wa "Kutafakari Upya Demokrasia ya Kiliberali ya Magharibi kwa Afrika" uliofanyika katika Maktaba ya Urais ya Olusegun Obasanjo katika mji mkuu wa Jimbo la Ogun, Abeokuta.

Rais huyo wa zamani wa Nigeria ameitafsiri demokrasia ya kiliberali ya Magharibi kama "serikali ya watu wachache juu ya watu wote au juu ya idadi kubwa ya watu" ambayo inapuuza maoni ya wengi. Amesema, mfumo huo wa utawala uliundwa bila kutilia maanani historia ya Kiafrika na tamaduni zake nyingi. Hekaheka za uchaguzi wa demokrasia ya Magharibi nchini Kenya

Obasanjo amefafanua kwa kusema: "tuna mfumo wa serikali ambao hatuna mchango wa kuuelezea wala kuusanifu, na tunaendelea kuwa nao hata tunapojua kwamba hauwezi kufanya kazi kwetu sisi,"

Rais huyo wa zamani wa Nigeria amependekeza kile alichokiita "demokrasia inayojikta kwenye Uafrika" itakayobuniwa kwa kuzingatia mahitaji ya bara la Afrika.

Ameendelea kueleza kwamba lazima Waafrika wahoji ufanisi wa demokrasia katika nchi za Magharibi, ambako ndiko ilikotoka na Afrika ambayo ni mrithi wa kile ilichoachiwa na mamlaka za kikoloni.

Obasanjo ametoa kauli hiyo ya ukosoaji wa demokrasia ya kiliberali ya Magharibi huku bara la Afrika likishuhudia wimbi la mchafukoge wa kisiasa, uliochochewa na mapinduzi ya kijeshi yanayoonekana kama mjibizo wa madai ya kushindwa viongozi waliochaguliwa kidemokrasia kutekeleza majukumu yao. Katika miaka mitatu iliyopita, mapinduzi manane ya kijeshi yametokea katika nchi za Afrika Magharibi na Kati, ya hivi karibuni zaidi yakiwa ni katika makoloni ya zamani ya Ufaransa ya Niger na Gabon.../

Chanzo: www.tanzaniaweb.live