Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

OG Himself: Khaligraph Jones aongoza wasanii kukutana na DP Ruto

51196b700b3c3355 OG Himself: Khaligraph Jones aongoza wasanii kukutana na DP Ruto

Mon, 26 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Khaligraph alikuwa ameomba DP Ruto kuingilia kati na kusaidia wasanii akisema wanaumia

- Alisema kafyu na kufungwa kwa maeneo ya burudani kumekuwa pigo kubwa kwa sekta yao

- Kwenye kikao cha Jumamosi DP alisema mapendekezo kadhaa yalitolewa kuhusu jinsi ya kukabili hali ya sasa

Naibu Rais William Ruto Jumamosi Aprili 24 alikutana na kundi la wasanii nchini wakiongozwa na Khaligraph Jones.

Khalighaph maarufu kama OG, jina halisi Brian Robert Ouko, alikuwa ameomba DP Ruto kutafuta suluhu kwa wasanii akisema wanaumia.

OG alimtaka DP kuhakikisha serikali inaondoa kafyu katika baadhi ya kaunti akisema wasanii wameathirika pakubwa.

Wakati wa kikao hicho cha Jumamosi, DP alisema walifanya kikao ili kupokea mapendekezo yao kuhusu hali ilivyo kwa sasa.



"Baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa ni kuundwa kwa mgao wa fedha kutoka kwa serikali ili kuwasaidia wasanii pamoja na kuhakikisha kuwa serikali inasaidia kufufua sekta hiyo," alisema DP Ruto.

DP alisema atahakikisha kuwa kilio cha wasanii kinashughulikiwa ili kusaidia waliokuwa wakijikimu kutokana na sekta hiyo.

Baadhi ya wasanii waliohudhuria kikao hicho ni msanii mkongwe Nonini, mcheza santuri Joe Mfalme na Willy Paul.

Tuko.co.ke ilikuwa imeripotia kwamba Jones aliahidi kumpigia Ruto kampeni 2022 bila malipo endapo atashinikiza kufunguliwa kwa taifa.

Mwanamuziki huyo alichapisha picha ya Ruto kwenye Instagram, akimtaja kama hastla na kuwasilisha kilio cha Wakenya.

Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kufungwa kwa maeneo yote ya burudani kuanzia Machi 12 kama njia moja ya kukabili ongezeko la maambukizi ya Covid-19.

Wasanii wengi wamekuwa wakiumia kwa sababu huchuma riziki katika maeneo ya burudani ambao wao hutumbuiza.

Wamekuwa wakiteta kuwa wanasiasa wanaendelea na shughuli zao huku wao wakifungiwa na hivyo kuachwa kuteseka.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke