Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Nzige waliopo Kusini mwa Ethiopia wanasambaa Afrika Mashariki" FAO

Mtanzanianews 137000195 139008017939767 1535630848481212218 N 660x400 "Nzige waliopo Kusini mwa Ethiopia wanasambaa Afrika Mashariki" FAO

Wed, 13 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), limeonya kuwa nzige walio Kusini mwa Ethiopia wanaanza kusambaa kuelekea katika mataifa ya Afrika Mashariki.

FAO katika ripoti yake iliyotolewa leo, inasema nzige hao wameanza kuonekana Mashariki mwa Ethiopia na baadhi ya maeneo ya Somalia, kuelekea Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Tayari nzige hao wapo katika kaunti za Kenya za Wajir, Garisa na Marsabit  lakini wenine wameonakana katika kaunti ya Taita Taveta, karibu na Tanzania.

Shirika hilo linaonya kuwa, kuendelea kuwepo kwa nzige hao kunatishia usalama wa chakula katika eneo la Afrika Mashariki, baada ya mwaka jana nchi za Afrika Mashariki kuharibu mabilioni ya wadudu hao.

AJALI LORI LA MAFUTA, TANKI LAPASUKA “WANANCHI WABISHI, WANATAKA KUCHOTA, POLISI WAMEWATIMUA”

Chanzo: millardayo.com