Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Nyumba za kuhifadhia maiti zimejaa zaidi,' joto kali laua zaidi ya 100 Mali

'Nyumba Za Kuhifadhia Maiti Zimejaa Zaidi,' Joto Kali Laua Zaidi Ya 100 Mali 'Nyumba za kuhifadhia maiti zimejaa zaidi,' joto kali laua zaidi ya 100 Mali

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Zaidi ya watu 100 wamekufa nchini Mali kutokana na joto kali lililoikumba nchi hiyo mwezi uliopita, ripoti zinasema.

Wiki iliyopita mji wa kusini-magharibi wa Kayes ulirekodi halijoto ya juu ya 48.5°C.

Itakuwa siku ya joto zaidi katika historia ya Afrika iliyorekodiwa mwezi Aprili, kulingana na wataalamu wa hali ya hewa waliotajwa na tovuti ya habari ya mtandaoni ya RFI.

Hospitali ya Gabriel-Toure katika mji mkuu, Bamako, ilipokea wagonjwa 102 walioathiriwa na joto ambao walikufa walipowasili, tovuti ya habari ya RFI ya Ufaransa iliripoti.

Wengi wao walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 60 na wagonjwa hali mahututi, Djibo Mahamane Django, mkuu wa idara ya ganzi hospitalini aliiambia radio ya eneo hilo Joliba FM

Vyanzo vingine vya habari viliweka idadi ya vifo kuwa zaidi ya 250 katika siku tatu.

"Tumeona ongezeko la idadi ya vifo, na vyumba vya kuhifadhia maiti vimejaa zaidi," Ladji Dibatéré, mmiliki wa nyumba za kuhifadhia maiti, alinukuliwa akisema.

Bw Dibatéré alisema familia zinalazimika kuweka miili ya jamaa zao nyumbani.

Maafisa wamewataka wakaazi kusalia katika maeneo yenye hewa ya kutosha na kuwawekea vikwazo watoto wa shule kwani vijana na wazee ndio walio hatarini zaidi, kituo cha televisheni cha ORTM kinachomilikiwa na serikali ya Mali kiliripoti.

Mamlaka imefupisha na kubadilisha saa za shule kwa wanafunzi wa shule ya msingi ili kuwalinda kutokana na kiwango cha juu cha joto.

Joto la juu limechangiwa na hali ya hewa ya El Nino, ambayo imeongeza joto la bahari na anga.

Utawala wa kijeshi wa Mali bado haujatoa maoni juu ya kuongezeka kwa joto.

Chanzo: Bbc