Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyuki Wavamia Mazishi na Kuua Mtu

Nyuki Kimbia Watu wakikimbia nyuki.

Wed, 29 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KATIKA hali ya kushangaza, kundi kubwa la nyuki wamevamia ghafla eneo la mazishi huko Gatundu Kaskazini mwa Kaunti ya Kiambu nchini Kenya na kuua muombolezaji mmoja.

Tukio hilo la aina yake limejiri Jumamosi, Septemba 25, 2021 ambapo waombolezaji walikuwa wakiendelea na shughuli ya mazishi na kumshambulia hadi kumuua mzee aliyefahamika kwa jina la Mungai Mburu ambaye alikuwa mzee wa kijiji wakati wa maziko ya mjukuu wake.

Imeelezwa kuwa, mke wake marehemu, Bi. Wanjiku Mburu baada ya maombi kufanyika kwenye kaburi la marehemu, nyuki waliwavamia na kuwasambaratisha waombolezaji huku kila mmoja akichanja mbuga kuokoa maisha yake.

Wanjiku ameeleza kwamba ni katika taharuki hiyo ndipo mume wake aliyekuwa na umri wa miaka 85, alianguka chini baada ya kusukumwa na umati wa watu na kukumbana na mauti yake mikononi mwa nyuki hao.

Juhudi za wasamaria wema kujaribu kuokoa maisha yake hakizikufua dafu kwani alithibitika kufariki alipofikishwa katika Hospitali ya Igegania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live