Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyeri: Msichana aliyedanga kutekwa nyara akamatwa akiwa kwenye baa

Fec2d782ab5ec936 Nyeri: Msichana aliyedanga kutekwa nyara akamatwa akiwa kwenye baa

Fri, 26 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Msichana kutoka kaunti ya Nyeri aliyemdanganya mamake kwamba alikuwa ameteka nyara na watu wasiojulikana amekamatwa na maafisa wa upelelezi kutoka idara ya DCI.

Clare Muthoni alikuwa amempigia mamake simu na kumweleza kwamba watekaji nyara walitaka fidia ya KSh 30, 000 ndiposa wamuachilie huru la sivyo wangemkata shingo kwa kisu.

Muthoni pia alimuoonya mamake kupitia kwenye SMS dhidi ya kupiga ripoti kwa polisi akihofia kuuawa.

Akiwa mwingi wa wasi wasi mkubwa Jane Wamuyu ambaye ni mkaaji wa Satellite mtaani Riruta, alifululiza hadi katika kituo cha polisi cha Karen ambapo aliripoti kisa hicho.

Kulingana na maafisa wa DCI, Muthoni alikamatwa Ijumaa, Machi 26 akiwa kwenye baa na rafiki yake alitambulika kwa majina kama Diana Wanjiku.

" Ili kuthibitisha kwamba Muthoni alikuwa ametekwa nyara, alimtumia mamake picha kadhaa akiwa amefungwa miguu na mikono kwa kamba, akiwa ameketi sakafuni. Muthoni pia alikuwa ameweka kisu kando yake," Ripoti ya DCI ilisoma.

" Mshukiwa pia alikuwa amemtishia mamake dhidi ya kuwahusisha maafisa wa polisi la sivyo angeuawa hata hivyo mama huyo hakuwa na pa kukimbilia ila katika kituo cha polisi cha Karen," Ripoti hiyo ilieleza zaidi.

Baada ya kupiga ripoti, makachero walianzisha uchunguzi na wakawanasa wawili hao katika kijiji cha Misiani eneo la Kangudo wakiburudika kwa baa.

Aidha, ilibainika kwamba washukiwa hao hawakuwa wametekwa nyara ila walikuwa wametoroka mjini Nyeri ambapo wawili hao wanaishi.

" Makachero waligundua kwamba Muthoni alikuwa amepanga njama na rafiki yake wamdanganye mamake kwamba ametekwa nyara ili alipe fidia ya KSh 30,000 lakini njama yao haikufaulu," Ripoti hiyo ilielezea zaidi.

Hata hivyo, DCI imesema washukiwa hao wako kizuizini na wanasubiri kufikishwa mahakamani.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke