Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyati, mamba kuzifurusha familia za Msumbiji

Nyati, Mamba Kuzifurusha Familia Za Msumbiji Nyati, mamba kuzifurusha familia za Msumbiji

Fri, 26 May 2023 Chanzo: Bbc

Zaidi ya familia 1,000 zinatazamiwa kuhama makazi yao katikati mwa Msumbiji kufuatia mashambulizi ya wanyama pori.

Mkuu wa utawala wa eneo hilo katika wilaya ya Marromeu katika jimbo la Sofala alisema serikali ya eneo hilo itahamisha familia 1,500 zilizotishiwa na mashambulizi hayo.

Henriqueta de Rosário alisema mamlaka imerekodi vifo vya watu watatu kutokana na mashambulizi ya wanyamapori katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

Nyati kutoka Hifadhi Maalum ya Marromeu katika delta ya mto Zambezi wamevamia maeneo ya makazi na kuwalazimu wakazi kuhamia visiwa vya mto huo.

Hata hivyo, wanapotafuta hifadhi visiwani humo, wanakabiliwa na tisho la kushambuliwa na mamba.

"Mgogoro kati ya mwanadamu na wanyamapori ni ukweli unaokua" alisema Bi Rosário, akiongeza kuwa watu wengi walitishiwa.

Alisema kuwa takriban watu 400 tayari walikuwa wamejiandikisha kwa ajili ya mpango wa makazi mapya ya hiari ili kuondoka katika eneo hilo.

Chanzo: Bbc