Nchi kumi za Kiafrika zinachangia 46% ya kesi za Omicron zilizoripotiwa ulimwenguni, Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani.
WHO inasema nchi nyingi kati ya hizi ziko kusini mwa Afrika, ambapo wanasayansi wanakuwa waangalifu zaidi kwa kesi zingine na wanachunguza sampuli ili kuangalia mabadiliko ya virusi.
Shirika hilo limesema nchi nyingi kati ya hizi ziko kusini mwa Afrika, ambapo wanasayansi wanakuwa waangalifu zaidi kwa visa vingine na wanachunguza sampuli ili kuangalia mabadiliko ya virusi.
Viwango vya kulazwa hospitalini na visa vya maambukizi makali yanasalia chini nchini Afrika Kusini, data ya ndani inaonyesha. Lakini utafiti bado unaendelea.
"Hakuna vifo vilivyohusishwa na kirusi kipya cha Omicron na marufuku ya usafiri haitazuia kusambaa kwake"
Kupata chanjo mikononi mwa watu kutazuia virusi hivyo kubadilika zaidi, inasema WHO, lakini barani Afrika, ni Mauritius, Morocco, Tunisia, Ushelisheli, Cape Verde na Botswana pekee ndio wamefikia lengo la kimataifa la kuchanja asilimia 4 ya watu wao kufikia mwisho wa mwaka huu.
Nchi nyingi za Kiafrika bado hazijatoa dawa kwa sababu ya vifaa, wakati mashaka ya umma kuhusu kupata chanjo hiyo bado ni kikwazo.