Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

North Korea kupanua uhusiano na nchi za Afrika

Kiduku Korea North Korea kupanua uhusiano na nchi za Afrika

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOREA Kaskazini imesema siku ya ya Alhamisi kuwa inakusudia kuboresha uhusiano wake wa zamani na mataifa ya Afrika na kuapa kupanua uhusiano huo wa "urafiki na ushirikiano."

"Tumejitolea kuziunga mkono kikamilifu nchi za Afrika katika juhudi zao za kufikia amani, utulivu na uadilifu wa kisiasa na kiuchumi wa bara hili na kujenga Afrika yenye ustawi kwa juhudi zao wenyewe na kukuza uhusiano wetu wa urafiki na ushirikiano na nchi za kanda," Alisema Song Se-il, rais wa Jumuiya ya Korea Kaskazini-Afrika.

Taarifa hiyo ya lugha ya Kiingereza, iliyotolewa kwenye tovuti ya wizara ya mambo ya nje ya Pyongyang, ilikuja wakati Afrika ikiadhimisha miaka 60 ya Siku ya Afrika, ambayo inaadhimisha msingi wa Umoja wa Afrika ulianzishwa Mei 25, 1963.

Se-il amezitaja nchi kama Madagascar, Guinea ya Ikweta, Uganda na Sierra Leone, kuwa uhusiano wa kirafiki wa Pyongyang na bara hilo ulianza tangu enzi za mwanzilishi wa eneo la Kaskazini marehemu Kim Il-sung.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live