Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Njaa yaua watu 50 nchini Ethiopia huku kukiwa na ukame

Njaa Yaua Watu 50 Nchini Ethiopia Huku Kukiwa Na Ukame Njaa yaua watu 50 nchini Ethiopia huku kukiwa na ukame

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Zaidi ya watu 50 wamefariki katika maeneo ya kaskazini mwa Tigray na Amhara nchini Ethiopia kutokana na njaa iliyosababishwa na ukame, maafisa wa eneo hilo wameiambia BBC.

Kulingana na ofisi ya Tigray ya Kudhibiti Hatari ya Majanga, watu 46 waliokimbia makazi yao walikufa baada ya kuwa tayari wameacha makazi yao kwa sababu ya ukame.

Vifo hivyo vilitokea katika mji unaoitwa Yechila, mkuu wa ofisi hiyo Gebrehiwot Gebregziabher alisema.

Katika eneo jirani la Amhara la Wag Hemra, takriban watu sita na ng'ombe 4,000 wamekufa kwa sababu ya uhaba wa chakula uliosababishwa na ukame, afisa wa eneo hilo amesema.

Kwa zaidi ya miezi mitano, Marekani na Umoja wa Mataifa walikuwa wamesitisha msaada wa chakula kwa Ethiopia kufuatia madai ya wizi mkubwa.

Hii inazidisha mateso kibinadamu nchini humo ambapo vita na hali mbaya ya hewa iliwaacha mamilioni ya watu wakitegemea misaada.

Huku maeneo ya kaskazini mwa Ethiopia yakikabiliwa na ukame mkubwa, maeneo ya kusini na mashariki mwa nchi hiyo yanatarajiwa kukumbwa na mvua kubwa isiyo ya kawaida.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 40 wamefariki katika wiki za hivi karibuni kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi, wengi wao wakiwa katika eneo la mashariki mwa Somalia.

Chanzo: Bbc