Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nitawashinda asubuhi mapema!DP Ruto awaambia wapinzani wake wajiweke tayari

D2423300e1aba222 Nitawashinda asubuhi mapema!DP Ruto awaambia wapinzani wake wajiweke tayari

Sat, 23 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto amewataka wanasiasa wanaowania kiti cha urais kuwa na ujasiri na kuwaelezea Wakenya manifesto zao.

William Ruto alisema inachekesha kwamba wapinzani wake wa siasa wanakutana kwenye hoteli na migahawa badala ya kutangamana na watu ana kwa ana. Mwaniaji huyo wa Rais wa kambi ya Tangatanga aliwahimiza wafuasi wake kusalia ngangari huku akiahidi kuimarisha maisha yao.

Naibu huyo wa rais alidai kwamba wanaowania kiti cha urais waliingiwa na hofu kwa jinsi alivyozidi kuwa maarufu na kupata uungwaji mkono zaidi yao.

Ruto alishangaa ni kwa nini wapinzani wake wanaunda vikundi na kufanya mikutano kwenye hoteli na migahawa badala ya kuzungumza ana kwa ana na wananchi.

Akizungumza katika Kaunti ya Kakamega mnamo Ijumaa, Oktoba 22, Ruto aliwaalika wanaotaka kumrithi Rais Uhuru Kenyatta kushindana naye kwenye uchaguzi mkuu wa 2022.

"Wanapaswa kukoma kumpotezea Uhuru wakati, Uhuru sio mshindani wao, mimi ndiye mshindani wao. Wacha waje wakabiliane nami ana kwa ana. Wanapaswa kujipanga vilivyo na kuchagua mwaniaji urais atakayetueleza ana mipango gani kuhusu maendeleo. Kutushambulia kwa kuunga mkono mahasla haitoshi," Ruto alisema.

Ruto aliwahimiza wafuasi wake wanaounga mkono mahasla wawe ngangari huku akiahidi kuyabadilisha na kuimarisha maisha yao.

Huku akionekana kuongea kwa mafumbo, Ruto alisema kinara wa ODM Raila Odinga, kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, na kiongozi wa Amani National Congress Musalia Mudavadi, walionekana kuingiwa na hofu kwa jinsi ushawishi wake wa siasa ulivyozidi kuongezeka.

"Wanafaa kujiandaa kwa sababu ni wananchi ndio watakaofanya uamuzi nani atakuwa rais. Hao hawawezi kukabiliana nami, wanajua nitawashinda asubuhi mapema," Ruto aliuambia umati wa watu ulioonekana kuwa na msisimko katika soko la Khayega.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke