Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nitapunguza ushuru iwapo nitachaguliwa rais 2022, Mudavadi aahidi

16af6312ba4d8b66 Nitapunguza ushuru iwapo nitachaguliwa rais 2022, Mudavadi aahidi

Tue, 6 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kiongozi wa chama cha ANC, Musalia Mudavadi alisema serikali yake itazingatia kupunguza ushuru endapo atachaguliwa rais mwaka 2022 Mudavadi aliibua wasiwasi kuhusu hali ya sasa ya uchumi nchini akisema mengi yanatakiwa kufanywaHaya yanajiri baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutia saini Mswada wa Fedha 2020 kuwa sheria

Kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi amesema atazingatia kupunguza ushuru endapo atachaguliwa rais mwaka 2022.

Akizungumza Nakuru Jumapili, Julai 4, Mudavadi aliibua wasiwasi kuhusu hali ya sasa ya uchumi nchini akisema mwananchi wa kawaidia amesukumwa mzigo wa ushuru ghali na serikali.

Kigogo huyo alisema kuhimarisha uchumi ndio itaku kibarua chake cha kwanza punde atakapochaguliwa na Wakenya.

"Nilihudhuria Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Christ The King Cathedral Nakuru. Iwapo Mungu atanipa nafasi ya kuwa kiongozi wa taifa hili nitapunguza ushuru," alisema.

Mudavadi, ambaye ni mwanauchumi amekuwa akionyesha ari ya kutumia ujuzi wake wa uchumi kuwavizia wapigia kura akijaribu kuwania urais mara ya pili.

Uhuru atia saini mswada wa bunge Kauli ya Mudavadi inajiri baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutia saini Mswada wa Fedha 2020 kuwa sheria.

Sheria hiyo lifanyia marekebisho vipengele kadhaa kuhusu ushuru katia sekta ya fedha.

Hii ni ikiwemo Bima, Masoko, malipo ya uzeeni na Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru, (KRA)

Sheria hiyo ilianza kutekelezwa Julai 1.

Kutiwa saini kwa mswada huo ambao umeongeza ushuru wa mjazo wa simu za mkono, mikopo kutoka benki, bei ya gesi ya kupikiana elimu ya dijitali.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke