Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Ninajiuliza kwa nini wanaume hawawaoi wasichana wenye ulemavu wa macho’

MSICHANA MLEMAVU WA MACHO ‘Ninajiuliza kwa nini wanaume hawawaoi wasichana wenye ulemavu wa macho’

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Msichana mwenye ulemavu wa kutoona nchini Burundi Francine Niyonkuru anasema anajiuliza ni kwanini wanaume hawawatongozi wanawake wenye ulemavu wa macho.

Katika mahojiano na BBC, Bi Francine ambaye ni muhitimu wa Chuo anasema kuwa walemavu wanapokuwa shuleni wanafanya vyema sawa na wenzao wasio kuwa na ulemavu na mara nyingine hata kupata alama bora zaidi, akijitolea mfano yeye binafsi.

Hatahivyo anasema, changamoto inakuwa pale wanapomaliza masomo na kukosa wanaume wa kuwaoa.

"Wanaume wengine ni kama wamefunikwa kitambaa usoni, sijui wanafikiria nini…wanajiuliza aah! Siwezi kumuoa msichana asiyeona,niwa kulazwa, kuvalishwa, wanatuchukulia kuwa hatuna faida. Anaona atakuwa amejitwika mzigo. Sijui kama Mungu alipowaumba Adam na Eva alisema wasioona hawamo sijui," anauliza Bi Niyonkuru huku akicheka.

Anadai ni wasichana wachache wenye ulemavu wa kutoona ambao hupata wachumba wa kuwaoa.

Alipulizwa je anaweza kujielezea vipi kwa yule ambaye angependa kumuoa alisema: Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 23,mfupi , mwenye kilo nyingi, sina umbo zuri, lakini siwezi kukosa mwanaume wa kunipenda’’.

Florance anasema ni msichana anayependa kusoma sana, na anasema japoanakipaji cha uchekeshaji, ndoto yake ni kuwa mwandishi wa habari.

Chanzo: Bbc