Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nimonia chanzo cha kifo cha mwandishi

Rita Tinina Rita Tinina enzi za uhai wake.

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uchunguzi wa mwili wa mwandishi wa habari mkongwe wa kituo cha NTV Kenya, Rita Tinina, aliyekutwa amefariki dunia nyumbani kwake Machi 17 mwaka huu umebaini kuwa alipoteza maisha kutokana na nimonia kali.

Msemaji wa familia ya Rita Timothy Njaga, amesema uchunguzi wa mwili ulifanyika siku ya Jumanne ukiongozwa na daktari wa serikali Peter Ndegwa, pamoja na Dkt Michaka.

Familia hiyo imesema imeridhishwa na ripoti ya madaktari na kuomba wapewe faragha ili kumuomboleza mpendwa wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live