Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Nimekaa Bila Kukamatwa"Sonko Asema Ataingia Kiambaa Leo

14e3a35482fedd16 "Nimekaa Bila Kukamatwa"Sonko Asema Ataingia Kiambaa Leo

Thu, 15 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mike Sonko ametabiri kuwa leo itakuwa ni kamata kamata wakati wa uchaguzi mdogo wa KiambaaAlisema atakuwa Kiambaa kama wakala lakini ananukia huenda atakamatwaUshindani ni mkali sana kwenye kinyang'anyiro hicho huku Njuguna Wanjiku wa UDA akitoana kivumbi na Kariri Njama wa JubileeAliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko Jumatano Julai 14 alitabiri kuwa hali itakuwa mbaya wakati wa uchaguzi mdogo eneo bunge la Kiambaa.

Sonko aliashiria kuna wanasiasa wa mrengo fulani ambao watakamatwa huku akisema huenda akawa mmoja wao.

Kupitia kwa ukurasa wake wa Facebook, alisema ni muda tangu anuse pingu na seli za polisi na hivyo Julai 15 atakuwa Kiambaa.

Alisema atakuwa eneo hilo kama mmoja wa mawakala wa kuchunga kura za wagombea wanaomenyana katika kivumbi hicho.

"Nimekaa sana bila kuwekwa ndani kesho nitakuwa Kiambaa. Unafikiria nitakuwa wakala wa wanani?" aliuliza Sonko.

Read also

Picha Tamu za Gavana Hassan Joho na Ann Waiguru Wakijivinjari

Matamshi ya Sonko yalizua michango mseto huku wengi wakihisi kuwa polisi watahusika pakubwa wakati wa uchaguzi huo mdogo.

Kinyang'anyiro hicho ni kikali sana kati ya wagombea wa vyama vya United Democratic Alliance (UDA) na Jubilee Kariri Njama na Njuguna Wanjiku.

Ni uchaguzi ambao una umuhimu zaidi kisiasa kwa kila pande na hivyo wamejikakamua kuhakikisha kuwa wanaibuka washindi.

Umejitokeza kama mashindano ya kisiasa kati ya Rais Uhuru Kneyatta na naibu wake William Ruto na siasa za 2022.

Iwapo UDA itaibuka na ushindi, basi itakuwa ni mazishi kwa chama cha Jubilee na pia ishara ya kudidimia kwa ushawishi wa Rais katika siasa za Mlima.

Habari Nyinginge: Zaidi ya Watu 70 Waangamia Wakishinikiza Kuachiliwa kwa Rais wa Zamani Jacob Zuma

Wadadisi wanasema uchaguzi huo utakuwa na athari kwa wanasiasa wa Mt Kenya pia kwani watalazimika kufanya uamuzi kuhusu chama watakachoingia.



Read also

Jamal Rohosafi Ajibu Madai ya Mkewe Kwamba Hana Kitu : "Mungu Anashughulika"

Wale wa Jubilee watakuwa na nafasi ya kuendelea kujenga chama chao wakipata ushindi huku UDA ikitaraji kuvuna zaidi iwapo itawika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke