Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Niko tayari kufanya mjadala na Raila, William Ruto asema

1fe518fba7976b4e Niko tayari kufanya mjadala na Raila, William Ruto asema

Fri, 25 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ruto alisema hana tatizo lolote iwapo ataiwa kwenye mjadala na Raila kuhusu masaibu ya KenyaWawili hao ndio farasi wakuu kwenye mbio za Ikulu 2022 na wamegeuka kuwa mahasimu wakuuMjadala kati ya wawili hao utakuwa ni kivutio kwa Wakenya wengi kwani wamekuwa wakirushiana maneno makali tangu wapeane talaka 2007Naibu Rais William Ruto amesema yuko tyaari kufanya mjadala na Raila Odinga kuhusu ajenda zao kwa Wakenya wanapomezea mate kiti cha urais.

Mijadala ya wagombea wa urais huwa maarufu na ilifanyika mwisho Kenya 2013 ambapo wagombea wote walikutana na kujibu maswali kutoka kwa waratibu.

Akiongea kwenye mahojiano na runinga ya KTN, Ruto alisema yuko tayari kabisa kujadili masuuala yanayoathiri taifa pamoja na kiongozi huyo wa ODM.

"Sina tatizo kuhusu hilo hata kidogo. Niko tayari kabisa," DP alisema baada ya kuulizwa iwapo anaweza kubali kuwa kwenye 'presidential debate' na Raila.

Ruto na Raila wanaonekana kuwa farasi wakali kwenye kinyang'anyiro cha 2022 wakati ambapo Rais Uhuru atakuwa akiondoka mamlakani.

Ni jambo ambalo limewafanya kuwa mahasimu wakuu wa siasa na hushambuliana kupitia kwa vyombo vya habari.

Ruto amekuwa akimlaumu Raila akisema ndiye chanzo cha masaibu yaliyokumba chama cha Jubilee.



"Kama nilivyosema 2017, bado hawana mpango wowote, Sasa wanaitwa watu wakubomoa kwa sababu walibomoa NASA na sasa wameleta matatizo ndani ya chama chetu cha Jubilee. Na saa hii hawajui walipo ama watakapoenda," alisema Ruto kumhusu Railakwenye mojawapo wa mikutano yake.

Raila naye humrushia vijembe Ruto akimtaja kama kiongozi fisadi ambaye anajitajirisha na mali ya umma.

"Kuna hawa ambao wanaiba mali ya umma na kisha wanaanza kuzunguka wakitoa michango kwa kina mama na vijana, harambee kanisani na mabasi kwa shule," alisema Raila wakati wa mazishi ya mfanyibiashara Chris Kirubi.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke