Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Night Club' yafungwa kwa madai ya ubaguzi wa rangi

Ubaguzi Wa Rangi Klabu 'Night Club' yafungwa kwa madai ya ubaguzi wa rangi

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu maarufu ya muziki jijini Nairobi Alchemist Bar, imetangaza kufungwa kwa siku chache ili kupisha uchunguzi baada ya video kusambaa mtandaoni ikimuonyesha mtu mweusi akizuiliwa kutoka kwenye foleni iliyokuwa na watu weupe na Waasia. .

Siku ya Jumatatu, watumiaji wa mtandao wa Twitter walitoa wito wakitaka kukomeshwa kwa madai ya ubaguzi wa rangi.

Lakini klabu hiyo ilikanusha kuwabagua watu weusi.

Katika taarifa yake Jumanne, The Alchemist Bar ilisema kuwa imeshauriana na serikali ya kaunti ya Nairobi na "itafunga milango yake , huku uchunguzi wa kina ukifanywa kwa muda wa siku chache zijazo".

Klabu hiyo ilisema itachunguza matukio ya usiku wa tarehe 20 Mei, ili kubaini ikiwa mtu huyo mweusi alikataliwa kuingia katika klabu hiyo na kama mistari tofauti ya wageni ilikuwa sehemu ya sera.

Pia inataka kubaini ikiwa kumekuwa na ubaguzi katika majengo kwa kukagua mahojiano na picha za matukio ya zamani.

Taarifa hiyo ilisema kuwa serikali ya kaunti ya Nairobi itaamua hatua zinazofuata baada ya matokeo ya uchunguzi huo.

Klabu hiyo ilisema itaajiri timu mpya ya usalama na kuweka mifumo ambayo itahakikisha kila mtu anakaribishwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live