Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria yaweka amri ya kutotoka nje ya saa 24 baada ya chakula kuporwa

Nigeria Yaweka Amri Ya Kutotoka Nje Ya Saa 24 Baada Ya Chakula Kuporwa Nigeria yaweka amri ya kutotoka nje ya saa 24 baada ya chakula kuporwa

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Gavana wa jimbo la kaskazini-mashariki la Adamawa nchini Nigeria ametangaza amri ya kutotoka nje ya saa 24 kufuatia uporaji wa maduka ya vyakula na maghala katika mji mkuu wa jimbo hilo, Yola.

Mamia ya watu walinaswa kwenye video, wakivunja maghala, wakibeba magunia ya nafaka, katoni za pasta na vitu vingine vya nyumbani.

Kwa amri ya Gavana Ahmadu Umaru Fintiri, maafisa wa usalama wametumwa kutekeleza amri ya kutotoka nje.

Mwezi uliopita, Nigeria ilimaliza utaratibu wa kutoa ruzuku ya mafuta, na kusababisha kupanda kwa bei ya vyakula na petroli.

Uchumi pia umedhoofishwa na mdororo wa uchumi na kuzorota kwa janga la Covid.

Chanzo: Bbc