Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria yatumbukia gizani huku wafanyakazi wakigoma

Nigeria Yatumbukia Gizani Huku Wafanyakazi Wakigoma Nigeria yatumbukia gizani huku wafanyakazi wakigoma

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Mamilioni ya Wanigeria hawana umeme baada ya gridi ya taifa kuzimwa kama sehemu ya mgomo wa taifa kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha. Nchi ilitumbukia gizani muda mfupi baada ya saa 02:00 kwa saa za ndani (01:00 GMT) wakati wanachama wa vyama vya wafanyakazi walipozuia wahudumu katika vyumba vya kudhibiti umeme nchini kufanya kazi na kuzima vituo vidogo vya umeme.

Safari nyingi za ndege pia zimesitishwa katika uwanja wa ndege wenye shughuli nyingi zaidi nchini humo mjini Lagos, na katika mji mkuu, Abuja, huku abiria wakiwa wamekwama.

Vyama vya wafanyakazi vinadai nyongeza kubwa ya kima cha chini cha mshahara, vikisema wafanyakazi hawawezi kuishi kwa kiwango cha sasa cha naira 30,000 sawa na dola 22 za kimarekani kwa mwezi.

Serikali inajitolea kuongeza hili maradufu lakini mlinzi Mallam Magaji Garba anaambia BBC kwamba hii haitatosha hata kununua gunia la kilo 50 la mchele, ambalo anahitaji kulisha familia yake kila mwezi.

Mfuko wa mchele hugharimu $56 - zaidi ya pendekezo la serikali, hata kabla ya kuzingatia matumizi mengine. "Ninatoa wito kwa serikali itufikirie na kuongeza kima cha chini cha mshahara ili tuweze kuishi na kula chakula kizuri," asema Bw Magaji, ambaye anafanya kazi katika wizara ya elimu katika jiji la kaskazini la Kano.

"Sio haki kwamba tuna maafisa wakuu wa serikali wanaopata mamilioni kila mwezi na wafanyikazi wadogo wanalipwa mshahara ambao hauwezi kukidhi mahitaji yao." Mzee huyo wa miaka 59 alisema wakati mwingine hulazimika kutembea kwa miguu kwenda kazini kwani hana uwezo wa kulipia usafiri.

Chanzo: Bbc