Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria yathibitisha kesi ya kwanza ya ugonjwa wa kimeta

 Kimeta Nigeria yathibitisha kesi ya kwanza ya ugonjwa wa kimeta

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Miji ya Nigeria amethibitisha rasmi kuhusu kesi ya kwanza ya ugonjwa wa kimeta kupitia taarifa iliyotiwa saini na Afisa Mkuu wa Mifugo wa Nigeria, Columba Vakuru.

Afisa Mkuu wa Mifugo wa Nigeria ameeleza kuwa ofisi yake ilipokea taarifa tarehe 14 mwezi huu kuhusu uwepo wa wanyama wenye dalili za uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa wa kimeta katika shamba la Suleja katika jimbo la Niger nchini humo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, baadhi ya wanyama katika shamba hilo tajwa walikuwa na dalili za kutokwa damu katika matundu ya miili yao kama puani, masikioni na kwingineko.

Baadhi ya dalili za kimeta ambazo huwa nazo mtu aliyeambukizwa ni kama zifuatazo: Homa na baridi, maumivu ya kichwa, kuvimba kwa tezi za shingo au shingo lenyewe, maumivu ya koo, kumeza kwa uchungu, kutapika n.k

Kimeta ni ugonjwa mbaya wa kuambukiza unaosababishwa na bakteria kwa jina Bacillus Anthracis. Ugonjwa huu huwaathiri binadamu na wanyama, ikiwa ni pamoja na wanyama wa porini na wale wanaofugwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kama ng'ombe, kondoo, mbuzi, nk.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live