Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria yasaini mikataba mipya ya kibiashara na Ujerumani

Nigeria Yasaini Mikataba Mipya Ya Kibiashara Na Ujerumani Nigeria yasaini mikataba mipya ya kibiashara na Ujerumani

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: Voa

Rais wa Nigeria Bola Tinubu anakaribisha mikataba mipya ya kibiashara na Ujerumani, ikijumuisha makubaliano ambayo yanalitaka taifa hilo la Afrika Magharibi kusafirisha gesi asilia.

Jumanne ilitiwa saini mikataba miwili ya maelewano kati ya makampuni ya Nigeria na makampuni ya Ujerumani, ni miongoni mwa msururu wa mikataba ya hivi karibuni ya uwekezaji iliyothibitishwa na utawala wa Tinubu katika miezi ya hivi karibuni.

Utiaji saini huo unakuja chini ya wiki mbili baada ya Nigeria na Saudi Arabia kufanya makubaliano ya kufufua mitambo isiyofanya kazi nchini humo.

Tinubu anataka kuifanya Nigeria ivutie wawekezaji katika jitihada za kufufua uchumi ulioathiriwa na ukuaji hafifu, mfumuko wa bei na madeni makubwa.

Chini ya mpango mmoja, Riverside LNG ya Nigeria itasambaza tani 850,000 za gesi asilia iliyoyeyushwa kwa Ujerumani kila mwaka, ikifanya kazi na kampuni ya Ujerumani Johannes Schuetze Energy Import AG.

Uwasilishaji wa kwanza wa gesi unatarajiwa mnamo 2026, na ofisi ya rais ilisema mauzo ya gesi yanaweza kuongezeka katika miaka ijayo.

Mamlaka zinasema makubaliano hayo yataifanya gesi asilia ambayo vinginevyo ingewashwa angani itumike. Nigeria ni nchi yenye akiba kubwa sana ya gesi barani Afrika - zaidi ya kubik mita za ujazo trilioni tano - lakini kutokana na miundombinu duni ya mchakato, nchi hiyo inapoteza idadi kubwa ya gesi kila siku.

Chanzo: Voa