Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria yapewa maagizo kurejesha umeme Niger

Umeme 1 660x384 Nigeria yapewa maagizo kurejesha umeme Niger

Sun, 13 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakili mwandamizi nchini Nigeria na mwanaharakati wa haki za binadamu Femi Falana ametoa wito kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) , kurejesha umeme nchini Niger na kupunguza vikwazo vilivyowekwa kwa nchi hiyo kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya hivi karibuni.

Falana amesisitiza kwamba raia wa kawaida wa Niger ndio wanaoteseka zaidi kutokana na hatua za adhabu, ikiwa ni pamoja na kukatwa kwa umeme, akibainisha kuwa viongozi wa kijeshi wanatumia majenereta kukidhi mahitaji yao binafsi ya umeme..

Falana amenukuliwa na vyombo vya habari akisema: "Katika kutekeleza vikwazo vya kiuchumi, utawala wa Bola Tinubu [Rais wa Nigeria ambaye pia ni mwenyekiti wa ECOWAS] umepunguza usambazaji wa umeme kwa Jamhuri ya Niger na hatua hizo zimekuwa na matokeo mabaya kwa raia. Kwa maneno mengine, raia wametupwa gizani ingawa hawakuhusika katika kupanga na kutekeleza mapinduzi hayo."

Mwanaharakati huyo pia amesema kuwa "kukatwa kwa umeme hakuna athari mbaya kwa viongozi wa utawala wa kijeshi Niger. Rais Tinubu anapaswa kuelekeza Tume ya Udhibiti wa Umeme ya Nigeria kurejesha umeme nchini Niger mara moja."

Hayo yanajiri wakati ambao serikali ya Russia imepinga uingiliaji wa kijeshi katika nchi ya magharibi mwa Afrika ya Niger ikisisitiza kuwa, uingiliaji wowote wa kijeshi nchini humo utazidi kuvuruga usalama wa eneo la Sahara-Sahel, lakini wakati huo huo imeunga mkono juhudi za kidiplomasia za kuutatua kwa amani mgogoro huo.

Kiongozi wa kijeshi Niger, Abdourahmane Tchiani Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema, inaunga mkono juhudi za upatanishi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) nchini Niger ambako tarehe 26 mwezi uliopita wa Julai, wanajeshi walimpindua Rais Mohamed Bazoum na wanamshikilia hadi hivi sasa.

Nchi za Magharibi hasa Marekani na Ufaransa zimepata pigo kutokana na kupinduliwa Bazoum ambaye wananchi wa Niger wanasema alikuwa kibaraka mkubwa wa madola ya Magharibi.

Licha ya Niger kuwa na utajiri mkubwa wa maliasili kama uranium, lakini imeendelea moja ya nchi maskini zaidi duniani huku utajiri huo ukikombwa na madola ya Magharibi hasa Ufaransa.

Tayari utawala wa kijeshi nchini Niger umetangaza serikali mpya ya mpito na kumteua Ali Lamine Zeine kuwa waziri mkuu wa muda na Baraza la Mawaziri lenye watu 21. Hiyo ni hatua kubwa muhimu iliyochukuliwa nchini Niger baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Julai 26.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live