Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria yaondoa vikwazo dhidi ya Niger na kufungua tena mipaka

Nigeria Yaondoa Vikwazo Dhidi Ya Niger Na Kufungua Tena Mipaka Nigeria yaondoa vikwazo dhidi ya Niger na kufungua tena mipaka

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ameondoa vikwazo vyote vya kiuchumi vilivyowekwa dhdi ya nchi jirani ya Niger, miezi minane baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Aliamuru kufunguliwa mara moja kwa mipaka, kuanza tena kwa safari za ndege za kibiashara na usambazaji wa umeme nchini Niger.

Mauzo ya nje yakiwemo mifugo na vitunguu kutoka Niger hadi Nigeria yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Niger inayotegemea bidhaa kutoka nje ya nchi pia imekumbwa na uhaba wa bidhaa muhimu, huku watu wanaoishi mpakani wakiathirika zaidi na vikwazo hivi.

Mwezi uliopita, shirika la kanda ya Afrika Magharibi, Ecowas, lilikubali kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Niger, Mali, Burkina Faso na Guinea ambazo zimekuwa chini ya utawala wa kijeshi miaka kwa miwili iliyopita.

Mali, Niger na Burkina Faso zilikuwa zimetangaza kujiondoa katika Jumuiya ya Ecowas baada ya vikwazo hivyo kuwekewa.

Rais aliyepinduliwa wa Niger Mohamed Bazoum amezuiliwa na viongozi wa kijeshi nchini Niger tangu mapinduzi ya Julai mwaka jana.

Chanzo: Bbc