Serikali nchini Nigeria imeidhinisha likizo ya uzazi ya wiki mbili kwa watumishi wa umma wa kiume.
Hii inaashiria mabadiliko makubwa katika sheria za utumishi wa umma nchini humo inakuja baada ya miaka kadhaa ya mjadala uliozunguka suala hilo.
Nae Mkuu wa Utumishi wa Umma wa Nigeria Folasade Yemi-Esan amesema kuwa likizo ya siku 14 ya uzazi itawawezesha baba na watoto wao wachanga "kushikamana vizuri".
Lakini pia amesema likizo hiyo watapewa wanaume ambao wenzi wao wamejifungua na wale ambao wameasili mtoto aliye chini ya miezi minne.
Kabla ya sera hii, ni wanawake tu walikuwa na haki ya likizo ya uzazi.
Kuanzishwa kwa likizo ya uzazi kwa wanaume nchini Nigeria kunakuja wakati wanaharakati wanaendelea kushinikiza akinababa kuhusika zaidi katika utunzaji wa watoto na kusaidia mama.