Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria yafunga shule za kifahari kutokana na unyanyasaji

Lead British Unyanyasaji Nigeria yafunga shule za kifahari kutokana na unyanyasaji

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafisa wa Nigeria wamefunga shule ya kifahari katika mji mkuu, Abuja, kutokana na visa vya uonevu vinavyohusisha baadhi ya wanafunzi, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Video nyingi za wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Lead British wakiwashambulia wanafunzi wenzao ziliibuka na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Jumatatu.

Video hizo zilizua shutuma kali mtandaoni huku wazazi wenye hasira wakionekana kuvamia shule.

Siku ya Jumanne, wakuu wa shule walitangaza kufungwa kwa shule hiyo kwa siku tatu ili kuwawezesha kuchunguza suala hilo.

Kabiru Musa, afisa mkuu wa elimu, aliambia tovuti ya habari ya Punch kwamba Waziri wa Masuala ya Wanawake nchini Uju Kennedy-Ohaneye aliamuru kufungwa kwa shule hiyo.

Katika taarifa yake, shule hiyo ilisema "ina wasiwasi mkubwa" kuhusu visa vilivyoripotiwa vya unyanyasaji, na kuahidi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo.

Shule hiyo, iliyoanzishwa mwaka wa 2007, inatoa mtaala wa Uingereza uliochanganywa na mfumo wa elimu wa Nigeria.

Imekadiriwa kuwa mojawapo ya shule za ada ya juu zaidi nchini Nigeria, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live