Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria yafunga matumizi ya ‘Twitter’

A5c7c6c5de0394aa813fc28de301492c.jpeg Nigeria yafunga matumizi ya ‘Twitter’

Sun, 6 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI ya Nigeria imesimamisha matumizi ya Twitter katika nchi hiyo kwa muda usiojulikana. Waziri wa Mawasiliano, Lai Mohammed, ameeleza.

Kufungiwa huko kwa Twitter kunatokana na kile kilichoelezwa kuwa ni maumizi yasio sahihi yanayolenga kufifisha ushirikiano na umoja wa Wanigeria uliopo hivi sasa.

Twitter wamesema tangazo hilo lililotolewa Ijumaa mwishoni mwa wiki, wamelizingatia kwa makini.

Hatua hiyo imefikiwa siku chache baada ya tweet ya Rais Muhammadu Buhari kuondolewa kwa madai ya kukiuka sheria na kanuni za mtandao huo. Serikali haikueleza sababu za kuondolewa huko kwa tweet ya Rais Buhari.

Hata hivyo, awali Waziri Mohammed aliulaumu uamuzi wa mtandao huo mkubwa wa Kimarekani kuondoa tweet ya Rais na kukiita kitendo hicho kwamba si cha haki.

Mtandao huo uliondoa tweet ya Rais Buhari mwenye miaka 78 Juni Mosi mwaka huu. Imewakumbusha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea Nigeria kati ya mwaka 1967-1970.

Msemaji wa Twitter alisema rais alichokiweka kwenye ukurasa wake kilikwenda kinyume na kanuni

za mtandao wao.

Ijumaa, Twitter ambayo mwezi uliopita ilitangaza kuwa makao yake makuu kwa Afrika ni Ghana, nchi Jirani na Nigeria, ilieleza kuwa inafanyia uchunguzi na itatoa taarifa watakapojua zaidi kuhusu zuio hilo. Hata hivyo mpaka Ijumaa jioni, Twitter ilikuwa ikifanya kazi nchini Nigeria.

Chanzo: www.habarileo.co.tz