Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria yaahirisha uchaguzi wa ugavana katika majimbo

Nigeria Yaahirisha Uchaguzi Wa Ugavana Katika Majimbo Nigeria yaahirisha uchaguzi wa ugavana katika majimbo

Thu, 9 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Tume ya uchaguzi nchini Nigeria imeahirisha uchaguzi wa magavana wa majimbo na mabaraza ya mitaa kwa wiki moja.

Kura hizo zilikuwa zimepangwa kufanyika Jumamosi. Sasa zitafanyika tarehe 18 Machi.

Upinzani nchini Nigeria ulikuwa umeomba kuangalia mashine za kielektroniki za kupiga kura, hata hivyo, mahakama ilikataa malalamiko yao.

Tume ya uchaguzi ilisema changamoto ya kisheria imechelewesha maandalizi na mashine hazitakuwa tayari kwa wakati.

Ni kawaida kwa uchaguzi kuchelewa nchini. Mnamo 2019, uchaguzi wa rais na bunge uliahirishwa kwa wiki moja.

Ni kawaida kwa uchaguzi kuchelewa nchini.

Mnamo 2019, uchaguzi wa rais na bunge uliahirishwa kwa wiki moja.

Baraza la uchaguzi lilitaja masuala ya vifaa.

Upinzani umepinga ushindi wa rais mteule Bolu Tinubu mwezi uliopita.

Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (INEC) ilianzisha Mfumo wa Ithibati ya Wapigakura wa Bimodal (BVAS) kwa mara ya kwanza kama sehemu ya teknolojia mpya iliyotumiwa katika uchaguzi wa mwaka huu katika jitihada za kuboresha uwazi.

Lakini makundi ya waangalizi na vyama vya upinzani vilisema ucheleweshaji mkubwa wa upigaji kura na kushindwa katika mfumo wakati wa kupakia hesabu kuliruhusu kutokea kwa dosari wakati wa uchaguzi wa rais.

Chanzo: Bbc