Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria yaagiza kurejeshwa kwa dawa ya kikohozi ya watoto 'yenye sumu'

Nigeria Yaagiza Kurejeshwa Kwa Dawa Ya Kikohozi Ya Watoto 'yenye Sumu' Nigeria yaagiza kurejeshwa kwa dawa ya kikohozi ya watoto 'yenye sumu'

Thu, 11 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Mdhibiti wa dawa nchini Nigeria ameagiza kurejeshwa kwa kundi la dawa ya kikohozi ya watoto ya Johnson & Johnson baada ya vipimo kuonyesha ilikuwa na "kiwango cha juu kisichokubalika" cha dutu yenye sumu na inayoweza kusababisha kifo.

Dutu hii, Diethylene glycol, "ilipatikana kusababisha sumu kali ya mdomo katika wanyama wa maabara," Shirika la Kitaifa la Kudhibiti Chakula na Dawa nchini Nigeria (Nafdac) lilisema Jumatano.

Iliongeza kuwa matumizi ya binadamu ya Diethylene glycol husababisha madhara ya sumu, ikiwa ni pamoja na maumivu ya tumbo, kutapika, kuhara, kushindwa kutoa mkojo, maumivu ya kichwa, kubadilika kwa akili, na kuumia kwa papo hapo kwa figo ambako kunaweza kusababisha kifo.

Dutu hii imehusishwa na vifo vya hivi majuzi vya makumi ya watoto nchini Cameroon na Gambia.

Vipimo vya maabara vya dawa ya maji ya watoto ya Benylin inayotakiwa kurejeshwa pia ilionyesha kuwa ilisababisha "sumu ya mdomo ya papo hapo kwa wanyama wa maabara", mdhibiti aliongeza.

Si kampuni ya Johnson & Johnson wala Kenvue - ambayo inamiliki chapa ya Benylin baada ya kujitenga na Johnson & Johnson mwaka jana- wametoa maoni kuhusu taarifa ya Nafdac.

Dawa hiyo ilitengenezwa nchini Afrika Kusini mnamo Mei 2021 na ilikuwa na tarehe ya kumalizika muda wa kutumika Aprili 2024.

Kifungashio cha dawa hiyo kimeandikwa inaweza kutumika kupunguza kikohozi na dalili za kifua kufungana na kutibu homa na hali zingine za mzio miongoni mwa watoto wenye umri wa kati ya miaka miwili na 12.

Chanzo: Bbc