Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria waomba Uingereza imuhurumie seneta aliyepatikana na hatia

Nigeria Waomba Uingereza Imuhurumie Seneta Aliyepatikana Na Hatia Nigeria waomba Uingereza imuhurumie seneta aliyepatikana na hatia

Thu, 4 May 2023 Chanzo: Bbc

Wabunge nchini Nigeria wamewaomba maafisa wa mahakama nchini Uingereza “kucheza na sheria ili kutoa huruma” kuhusiana na hukumu ya mwanasiasa wa Nigeria aliyepatikana na hatia ya usafirishaji haramu wa viungo vya binadamu.

Senata Ike Ekweremadu, mke wake pamoja na daktari "ambaye aliwasaidia’’ walipatikana na hatia mwezi Machi kwa njama ya kusafirisha viungo cha mwili, baada ya kumleta mwanaume mwenye umri wa miaka 21 nchini Uingereza kutoka Lagos.

Hukumu yao inatarajiwa kutolewa Ijumaa.

Spika wa bunge la wawakilishi nchini Nigeria, Femi Gbajabiamila, alimuelezea Ekweremadu kama "mtu mwema" ambaye hakuwahi kupatikana na hatia awali, huku akiomba ahurumiwe.

Bunge la Jumuiya ya kiuchumi ya nchi zilizopo magharibi mwa Afrika (Ecowas) pia limeandika barua kwa mamlaka za Uingereza zikitaka msamaha utolewe kwa mwanasiasa huyo aliyepatikana na hatia.

Vyombo vya habari vya Nigeria viliinukuu barua ya Spika wa Ecowas aliyomuandikia karani mkuu wa mahakama ya uhalifu ya Old Bailey iliyopo mjini London.

Ilisema kuwa ingawa Ecowas “inapinga ”uhalifu ambao Ekweremadu alipatikana nao, ina “amini kuwa funzo limetolewa”.

Barua hiyo pia ilimuelezea Ekweremadu kama “mtu muhimu katika kanda ya Ecowas”.

Chanzo: Bbc