Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria kuuza ndege za rais

Nigeria Ndege Nigeria kuuza ndege za rais

Wed, 3 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Nigeria inapanga kuuza ndege tatu za rais kati ya ndege kadhaa rasmi za rais ikiwa ni sehemu ya hatua za kupunguza gharama katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ambayo inakabiliwa na mdororo wa kiuchumi.

Kwa mujibu wa taarifa, Rais Bola Tinubu ameamuru ndege na helikopta za rais zipunguzwa. Kwa sasa Nigeria ina ndege sita na helikopta nne za rais na uamuzi umechukuliwa kuuza ndege tatu kutokana na wasiwasi wa kuongezeka kwa gharama za usimamizi.

Kumekuwa na malalamiko kuhusu gharama kubwa za kutunza ndege hizo ambapo taarifa zinasema Nigeria ilitenga angalau naira bilioni 80 (karibu dola milioni 60) kwa gharama jumla za za matengenezo kati ya 2016 na 2023.

Awali Nigeria ilijaribu kuuza ndege mbili za rais mwaka 2016 wakati wa utawala wa rais wa zamani Muhammadu Buhari lakini haikuweza kupata wanunuzi. Wanunuzi wa awali waliripotiwa kutoa dola milioni 11 kwa ndege ya Dassault Falcon 7x na ile ya Beechcraft Hawker 4000, badala ya bei ya ambayo serikali ilitaka ya dola milioni 24. Serikali ilikataa ofa hiyo.

Nigeria ambayo ni nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika imekumbwa na mzozo wa gharama za maisha tangu Rais Tinubu, ambaye aliingia madarakani mwezi Mei, kuondoa ruzuku ya mafuta kama sehemu ya mageuzi ya kupunguza nakisi ya bajeti. Hatua hiyo imesababisha maandamano mitaani na migomo nchi nzima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live