Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria kuisambazia gesi Ujerumani

Tinu Master Nigeria kuisambazia gesi Ujerumani

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nigeria na Ujerumani zimeingia mkataba ambao Nigeria inatarajiwa kuanza kuisambazia Ujerumani gesi asilia huku kwa upande wa Ujerumani itaongeza uwekezaji wa hadi dola milioni 500 katika sekta ya teknolojia na miradi ya nishati mbadala nchini Nigeria.

Katika mkataba huo wa maelewano uliotiwa saini na kampuni ya Nigeria inayohusika na mradi wa gesi asilia ya Riverside inayofanya kazi katika jimbo la Delta na kampuni ya Kawi ya Ujerumani, Nigeria kuanzia mwaka 2026 itasafirisha tani 850,000 za gesi asilia kila mwaka nchini Ujerumani, na baadaye kiwango hicho kitaongezeka hadi tani milioni 1.2.

Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya kawi ya Ujerumani Jonannes Schuetze amesema makubaliano hayo ni hatua muhimu kuelekea upatikanaji wa gesi zaidi nchini Ujerumani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live