Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria kuanza kutoa chanjo ya Mpox

Afrika Kusubiri Kwa Muda Mrefu Kupata Chanjo Ya Mpox.png Nigeria kuanza kutoa chanjo ya Mpox

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa, itaanza kutoa chanjo ya kukabiliana na virusi vya homa ya Mpox kuanzia Oktoba 8, baada ya uidhinishaji wa chanjo hiyo kukamilika nchini humo.

Nigeria imepokea shehena ya kwanza ya dozi 10,000 ya chanjo hiyo kutoka shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani wiki hii.

Msemaji wa shirika la maendeleo ya afya ya msingi nchini Nigeria, Remi Adeleke, amesema chanjo zilizowasili lazima zifanyiwe utafiti wa kimaabara nchini humo kwa kipindi cha wiki tatu na baadaye zitaanza kusambazwa katika majimbo matano ambako watu 4,750 watachanjwa, kila mmoja atapata dozi mbili katika muda wa siku 28.

Tayari Umoja wa Afrika umetangaza dharura ya afya ya umma ili kukabiliana na kuenea kwa kasi virusi katika bara zima.

Mpox ni ugonjwa wa virusi ambao umeathiri nchi nyingi na kusababisha kutangazwa hali ya dharura ya afya ya umma ya kimataifa.

Mpox huenezwa zaidi na mguso wa moja kwa moja kutoka kwa mnyama mgonjwa, akiwa na au bila dalili, hadi kwa mtu mwenye afya. Pia kuna maambukizi kutoka kwa mtu mgonjwa hadi kwa mtu mwenye afya. Pia hupitishwa kutoka kwa mama mgonjwa hadi kwa mtoto wake wakati wa ujauzito

Dalili huonekana siku 5 hadi 21 baada ya kuambukizwa na hujumuisha homa, maumivu ya mwili, nodi za lymph zilizovimba na vidonda vya ngozi. Ingawa hakuna matibabu maalumu, dawa za kuzuia virusi zinaweza kusaidia kudhibiti hali hiyo. Kesi nyingi ni nyepesi na ahueni hutokea ndani ya wiki chache.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live