Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Zaidi ya watu 40 wahofiwa kuuawa na wanamgambo

Jeshi La Nigeria Zaidi ya watu 40 wahofiwa kuuawa na wanamgambo

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Nigeria imelazimika kupelekea maafisa wa usalama katika jimbo la Benue nchini Nigeria baada ya kuzuka mapigano makali kati ya makundi hasimu ya wanamgambo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 40.

Vyombo vya habari vya eneo hilo vimeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mapigano hayo, ambayo yalianza juzi Jumanne, yameenea kwa kasi.

Shirika rasmi la Habari la Nigeria (NAN) nalo limethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, mapigano hayo yametokea kwenye eneo la Gbagir lililoko chini ya serikali ya mtaa ya Ukum huko Benue.

Wakaazi wa eneo hilo wameripotiwa kukwama katikati ya mapigano hayo ya umwagaji damu, huku vita vikizidi kuwa vikali kati ya makundi ya wanamgambo ambayo hayakutajwa majina.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa wengi wa wahanga wa mapigano hayo ni wanachama wa vikundi vya wanamgambo hasimu. Jeshi la Nigeria

Duru za ndani ya Nigeria zimesema kuwa mapigano hayo yalianza kwa sura ya shambulio la kulipiza kisasi lililofanywa na kundi moja la wanamgambo ambao waliamua kulipiza cha kuteswa baadhi ya wakaazi wa eneo hilo na jamii jirani.

Jana jioni jeshi la polisi huko Benue lilithibitisha kutokea tukio hilo na kusema kuwa, ni maiti wanane tu ndio waliokuwa wamepatikana kwenye eneo hilo hadi wakati inaripotiwa habari hii.

Catherine Anene, msemaji wa polisi wa jimbo hilo la Benue, amewaambia waandishi wa habari kwamba, maafisa zaidi wa kuinda usalama wametumwa kwenye eneo hilo ili kurejesha amani na hali ya kawaida.

Msemaji huyo wa jeshi la polisi la jimbo la Benue ameongeza kuwa, uchunguzi umeanzishwa kuhusu mapigano hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live