Waathiriwa walioachiliwa hivi majuzi wa utekaji nyara nchini Nigeria wanasema nyoka wanatumiwa kuwatia hofu ili kuongeza fidia.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la utekaji nyara, huku pesa nyingi zikiporwa.
Mtu mmoja aliyetekwa nyara aliliambia Shirika la Habari linalomilikiwa na serikali la Nigeria kwamba baadhi ya waathiriwa walipelekwa katika maeneo yanayojulikana kuwa na nyoka na kutupwa msituni.
Kwa maneno ya mmoja wao, "hapo ndipo mwathirika atawauliza marafiki na familia kuuza kila kitu ili kupata fidia - nyumba, magari, bidhaa, kila kitu".
Wahalifu na waathiriwa wote wako katika hatari ya kuumwa - na wengine huumwa.
Madaktari wa eneo hilo wamethibitisha kuwa baadhi ya waathiriwa wa utekaji nyara wamehitaji matibabu ya kuumwa na nyoka kufuatia baada ya kuachiliwa.