Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nigeria: Wapinzani kupinga matokeo Mahakamani

Rais Mteule Wa Nigeria Bola Tinubu Amtembelea Rais Buhari Wapinzani kupinga matokeo Mahakamani

Sun, 5 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majimbo sita yanayoongozwa na upinzani nchini Nigeria yameiomba mahakama ya juu kutupilia mbali matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, ukisema chombo cha kusimamia uchaguzi kilivunja sheria na kanuni zake wakati wa kuhesabu kura.

Majimbo sita kati ya 36 nchini Nigeria ya Adamawa, Akwa Ibom, Bayelsa, Delta, Edo na Sokoto yalisema kwenye fomu za mahakama zilizojazwa ya kuwa tume ya uchaguzi ilishindwa kuwasilisha matokeo kupitia mfumo wa kielektroniki unaokusudiwa kuonyesha uwazi.

Katika ombi lao wameiomba mahakama kutangaza kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa na mwenyekiti wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwa "yalikuwa batili, hayatambuwi, na hayana maana yoyote."

Mgombea wa chama tawala nchini Nigeria, Bola Tinubu ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi iliyopita.

Tume Huru ya Uchaguzi Nigeria (INEC) ilimtangaza Tinubu aliyegombea kupitia chama tawala cha All Progressives Congress (APC) kuwa mshindi wa uchaguzi urais, kwa kupata kura milioni 8.8, akifuatiwa na mshindani wake wa karibu Atiku Abubakar wa chama cha Peoples Democratic Party (PDP) aliye[ata kura milioni 6.9.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi Nigeria, mgombea wa Chama cha Leba, Peter Obi, aliiibuka wa tatu kwa kupata kura milioni 6.1 katika uchaguzi huo wa kutafuta mrithi wa Muhammadu Buhari aliyemaliza uongozi wake wa mihula miwili.

Serikali ya ijayo ya Bola Tinubu inakabiliwa na kibarua kigumu hasa vita dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram, ufisadi uliokithiri na uchumi ambao umeendelea kuzorota siku baada ya siku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live